Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo UTANGULIZI

UTANGULIZI
Mwandishi wa kitabu hiki cha mwisho cha Biblia anajitaja kuwa Yohane na kwamba yeye ni nabii. Mapokeo ya kanisa yanamwona mwandishi huyo kuwa Yohane Mtume. Kitabu hiki kimeandikiwa jumuiya saba za Kikristo huko Asia Ndogo (sasa Uturuki).
Yohane anatuhabarisha katika kitabu hiki cha pekee mfululizo wa matukio mbalimbali ambayo Yesu Kristo alimfunulia (1:1) akiwa amekumbwa na nguvu ya Roho wake Kristo au Roho wa Mungu. Kitabu chenyewe ni mojawapo ya vile vitabu vya mtindo fulani ambao lengo lake ni kuelezea mambo ya nyakati za mwisho (apokaliptiki) – tazama utangulizi wa Danieli na Zekaria. Nyakati kitabu hiki kilipoandikwa zilikuwa za taabu na mateso kwa jumuiya ya Wakristo. Kwa hiyo Wakristo hao wanatiwa moyo wasije wakakata tamaa; wanatangaziwa kwamba mwisho wa tawala dhalimu na potovu za ulimwengu umekaribia na kwamba utawala wa Mungu unaanza. Katika kueleza jambo hilo muhimu, mwandishi Yohane anaoneshwa matukio hayo mbalimbali na Yesu Kristo mwenyewe ambaye ni shahidi mwaminifu wa Mungu. Mengi ya mambo hayo yanajulishwa kwake kwa njia ya maono, picha na mifano. Jumuiya saba za waumini (kanisa) huko Asia Ndogo ni mfano wa kanisa lote duniani kote.
Ufafanuzi wa kitabu hiki kigumu umetolewa au kuelezwa kwa njia mbalimbali na wataalamu wa mafundisho ya Biblia; lakini kitovu cha tamko la kitabu chenyewe ni wazi: Wakati nguvu za uovu zinapoonekana kusambaa kila mahali, kutakuwa na ushindi thabiti wa uwezo na nguvu ya Mungu dhidi ya uovu. Mungu atawapatia watu wake ushindi mkuu kwa njia ya Yesu Kristo aliye peke yake Bwana na Mwokozi. Hapo ndipo kutakapokuwa na mbingu mpya na dunia mpya.

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo UTANGULIZI: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia