Wimbo Ulio Bora UTANGULIZI
UTANGULIZI
Katika Kiebrania kitabu hiki kinaitwa “Wimbo wa Nyimbo”, yaani wimbo mzuri kupita zote: “Wimbo Bora”.
Huu mkusanyo wa tenzi ambazo kwa jumla zazungumzia urafiki au upendo kati ya mume na mke unasemekana kwamba Solomoni ndiye mwandishi wake. Lakini kusema kweli mkusanyo huu ni wa nyakati za baadaye sana baada ya Solomoni.
Jambo la mapenzi kati ya mume na mke katika Israeli halikuwa jambo ambalo lilikuwa aibu kutaja. Tenzi hizi zilipata kufafanuliwa na waalimu wa Kiyahudi kwa maana ya upendo uliopo kati ya Mungu na watu wa Israeli na msingi wa ufafanuzi huo wanauona katika Hos 1–3; Yer 2:20-3:5. Katika nyakati za kwanzakwanza za jumuiya ya Wakristo tenzi hizi zilifafanuliwa kama mfano wa upendo kati ya Kristo na Kanisa lake (taz Efe 5:21-33).
Iliyochaguliwa sasa
Wimbo Ulio Bora UTANGULIZI: BHN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.