Sefania UTANGULIZI
UTANGULIZI
Sefania alihubiri ujumbe wa Mungu huko Yuda kati ya mwaka 640 na 620 K.K., wakati wa utawala wa mfalme Yosia wa Yuda mnamo mwaka 640-609 K.K.
Muhimu katika mahubiri yake ni kwamba Mungu atawaadhibu watu wa Yuda na Yerusalemu kwa sababu walitumikia miungu ya uongo. Wakati huo atakapowaadhibu ndio wakati ule unaotajwa kama “Siku ya Mwenyezi-Mungu”. Hata mataifa ya jirani na Yuda nayo pia yataadhibiwa. Lakini katika siku za usoni wakazi wa Yerusalemu watamtumikia Mungu, naye Mungu atawafanikisha tena watu wake.
Iliyochaguliwa sasa
Sefania UTANGULIZI: BHN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.