1 Mambo ya Nyakati 10:13-14
1 Mambo ya Nyakati 10:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Shauli alikufa kwa sababu ya kutokuwa mwaminifu; hakuwa mwaminifu kwani hakutii neno la Mwenyezi-Mungu na alikwenda kwa mwaguzi kumtaka shauri, badala ya kumwendea Mwenyezi-Mungu ili kumtaka shauri. Kwa sababu hiyo Mwenyezi-Mungu akamuua, na ufalme wake akampa Daudi mwana wa Yese.
1 Mambo ya Nyakati 10:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akampa Daudi, mwana wa Yese.
1 Mambo ya Nyakati 10:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akamgeuzia Daudi, mwana wa Yese.
1 Mambo ya Nyakati 10:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa BWANA. Hakulishika neno la BWANA, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, hakumuuliza BWANA. Kwa hiyo BWANA alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.