1 Wakorintho 10:15-17
1 Wakorintho 10:15-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nasema watu wenye ufahamu, amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. Je, kikombe cha baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja.
1 Wakorintho 10:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo. Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo.
1 Wakorintho 10:15-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! Si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.
1 Wakorintho 10:15-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)