1 Wakorintho 8:1-2
1 Wakorintho 8:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Yahusu sasa vyakula vilivyotambikiwa sanamu: Tunajua kwamba sisi sote tuna ujuzi, lakini ujuzi huo huwafanya watu wawe na majivuno; lakini mapendo hujenga. Anayefikiri kwamba anajua kitu, kwa kweli hajui chochote kama inavyompasa.
Shirikisha
Soma 1 Wakorintho 81 Wakorintho 8:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lolote bado, kama impasavyo kujua.
Shirikisha
Soma 1 Wakorintho 81 Wakorintho 8:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na kwa habari ya vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; Twajua ya kuwa sisi sote tuna ujuzi. Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga. Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.
Shirikisha
Soma 1 Wakorintho 8