1 Timotheo 2:11-15
1 Timotheo 2:11-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanawake wanapaswa kukaa kimya na kuwa wanyenyekevu wakati wa kujifunza. Mimi simruhusu mwanamke amfundishe au amtawale mwanamume; anapaswa kukaa kimya. Maana Adamu aliumbwa kwanza, halafu Hawa. Na wala si Adamu aliyedanganywa; bali mwanamke ndiye aliyedanganywa, akaivunja sheria ya Mungu. Hata hivyo, mwanamke ataokolewa kwa kupata watoto, kama akidumu katika imani, upendo, utakatifu na unyofu.
1 Timotheo 2:11-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe msikivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
1 Timotheo 2:11-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
1 Timotheo 2:11-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji. Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi.