2 Samueli 22:8-16
2 Samueli 22:8-16 Biblia Habari Njema (BHN)
“Hapo, dunia ikatetemeka na kutikisika, misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka, kwani Mungu alikuwa amekasirika. Moshi ulifuka kutoka puani mwake, moto uunguzao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake. Aliinamisha anga, akashuka chini; na wingu jeusi chini ya miguu yake. Alipanda kiumbe chenye mabawa na kuruka, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Alijizungushia giza pande zote, kifuniko chake kilikuwa mawingu mazito na mkusanyiko wa maji. Umeme ulimulika mbele yake, kulilipuka makaa ya moto. Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni, Mungu Mkuu akatoa sauti yake. Aliwalenga adui mishale, akawatawanya, alirusha umeme, akawatimua. Mwenyezi-Mungu alipowakemea, kutokana na pumzi ya puani mwake, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.
2 Samueli 22:8-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasukasuka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao. Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni. Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa. BWANA alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye Juu akaitoa sauti yake. Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatimua. Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
2 Samueli 22:8-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasuka-suka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao. Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni. Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa. BWANA alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake. Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatapanya. Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
2 Samueli 22:8-16 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yaliyowaka yakatoka ndani yake. Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mabawa ya upepo. Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani. Kutokana na mwanga wa uwepo wake mwanga wa radi ukatoka. Mwenyezi Mungu alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. Aliipiga mishale na kutawanya adui, akawafukuza kwa umeme mkubwa wa radi. Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Mwenyezi Mungu, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.