Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samueli 22:8-16

2 Samueli 22:8-16 BHN

“Hapo, dunia ikatetemeka na kutikisika, misingi ya mbinguni ikayumbayumba na kuruka, kwani Mungu alikuwa amekasirika. Moshi ulifuka kutoka puani mwake, moto uunguzao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake. Aliinamisha anga, akashuka chini; na wingu jeusi chini ya miguu yake. Alipanda kiumbe chenye mabawa na kuruka, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Alijizungushia giza pande zote, kifuniko chake kilikuwa mawingu mazito na mkusanyiko wa maji. Umeme ulimulika mbele yake, kulilipuka makaa ya moto. Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni, Mungu Mkuu akatoa sauti yake. Aliwalenga adui mishale, akawatawanya, alirusha umeme, akawatimua. Mwenyezi-Mungu alipowakemea, kutokana na pumzi ya puani mwake, vilindi vya bahari vilifunuliwa, misingi ya dunia ikaonekana.