Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Sam 22:8-16

2 Sam 22:8-16 SUV

Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka, Misingi ya mbinguni ikasuka-suka Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu. Kukapanda moshi kutoka puani mwake, Moto ukatoka kinywani mwake ukala; Makaa yakawashwa nao. Aliziinamisha mbingu akashuka; Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake. Akapanda juu ya kerubi akaruka; Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo. Akafanya giza hema zake za kumzunguka, Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni. Toka mwangaza uliokuwa mbele zake Makaa ya moto yakawashwa. BWANA alipiga radi toka mbinguni, Naye Aliye juu akaitoa sauti yake. Akapiga mishale, akawatawanya; Umeme, naye akawatapanya. Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.