Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Samweli 22:8-16

2 Samweli 22:8-16 NENO

Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yaliyowaka yakatoka ndani yake. Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mabawa ya upepo. Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani. Kutokana na mwanga wa uwepo wake mwanga wa radi ukatoka. Mwenyezi Mungu alinguruma kutoka mbinguni, sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika. Aliipiga mishale na kutawanya adui, akawafukuza kwa umeme mkubwa wa radi. Mabonde ya bahari yalifunuliwa, na misingi ya dunia ikawa wazi kwa kukaripia kwake Mwenyezi Mungu, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.