Danieli 11:1-4
Danieli 11:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“ ‘Lakini kwa upande wangu mimi, katika mwaka wa kwanza wa mfalme Dario Mmedi, nilijitoa kumthibitisha na kumtia nguvu. Sasa nitakueleza ule ukweli wa mambo haya. “ ‘Tazama, wafalme wengine watatu wataitawala nchi ya Persia. Hao watafuatwa na mfalme wa nne ambaye atakuwa tajiri kuliko wale waliomtangulia. Wakati wa kilele cha nguvu na utajiri wake, ataanza kuushambulia ufalme wa Ugiriki. Kisha atatokea mfalme hodari atakayetawala eneo kubwa na kufanya atakavyopenda. Hata hivyo, wakati wa kilele cha uwezo wake, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu nne kuelekea pepo nne za mbingu. Wazawa wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa mikononi mwa milki aliyotawala, kwa sababu ufalme wake utachukuliwa na wengine.
Danieli 11:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa upande wangu, katika mwaka wa kwanza wa Dario, Mmedi, mimi nilisimama ili kumsaidia na kumtia nguvu. Nami sasa nitakuonesha yaliyo kweli. Tazama, watasimama wafalme watatu katika Uajemi; naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Ugiriki. Na mfalme hodari atasimama, atakayetawala kwa uwezo mkuu, na kutenda apendavyo. Naye atakaposimama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo; kwa maana ufalme wake utang'olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao.
Danieli 11:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena mimi, katika mwaka wa kwanza wa Dario, Mmedi, mimi nalisimama nimthibitishe na kumtia nguvu. Nami sasa nitakuonyesha yaliyo kweli. Tazama, watasimama wafalme watatu katika Uajemi; naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Uyunani. Na mfalme hodari atasimama, atakayetawala kwa mamlaka kubwa, na kutenda apendavyo. Naye atakaposimama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo; kwa maana ufalme wake utang’olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao.
Danieli 11:1-4 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Nami katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario Mmedi, nilisimama kumsaidia na kumlinda.) “Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme wengine watatu watatokea Uajemi. Kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi ya ufalme wa Uyunani. Ndipo mfalme mwenye nguvu atatokea, atakayetawala kwa nguvu nyingi, na kufanya anavyopenda. Baada ya kujitokeza, himaya yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautaenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizokuwa nazo, kwa sababu himaya yake itang’olewa na kupewa wengine.