Kumbukumbu la Sheria 10:12-13
Kumbukumbu la Sheria 10:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sasa, enyi Waisraeli, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu anataka nini kwenu, ila kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kuzifuata njia zake zote, kumpenda, kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na kwa roho zenu zote, na kuzitii amri na masharti ya Mwenyezi-Mungu ninayowawekea leo, kwa manufaa yenu wenyewe?
Kumbukumbu la Sheria 10:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzishika amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?
Kumbukumbu la Sheria 10:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote; kuzifuata amri za BWANA na sheria zake, ninazokuamuru leo, upate uheri?
Kumbukumbu la Sheria 10:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Na sasa, ee Israeli, BWANA Mungu wako anataka nini kwako ila kumcha BWANA Mungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikia BWANA Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na kuyashika maagizo ya BWANA na amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?