Esta 10:1-3
Esta 10:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme Ahasuero alitoza kodi watu wa bara na pwani. Matendo yake yote makuu na ya ajabu, pamoja na simulizi kamili kuhusu jinsi alivyompandisha cheo Mordekai na kumtunukia heshima kuu, yote yameandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za wafalme wa Media na Persia. Mordekai, Myahudi, alikuwa wa kwanza chini ya mfalme Ahasuero katika madaraka. Alipendwa na kuheshimiwa na Wayahudi, maana aliwafanyia mema watu wake na kuwatakia amani wazawa wao wote.
Esta 10:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari. Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi? Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.
Esta 10:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari. Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi? Kwa maana Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwatafuta watu wake wema, na kuiangalia hali njema ya wazao wao wote.
Esta 10:1-3 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika himaya yake yote, hadi miambao yake ya mbali. Na kuhusu matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amempandisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi? Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa na mkuu miongoni mwa Wayahudi. Aliheshimiwa sana na Wayahudi wenzake wengi, kwa sababu alifanya kazi kwa manufaa ya watu wake na kutetea ustawi wa Wayahudi wote.