Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Esta 10

10
Ukuu wa Mordekai
1Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika himaya yake yote, hadi miambao yake ya mbali. 2Na kuhusu matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amempandisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi? 3Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo baada ya Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa na mkuu miongoni mwa Wayahudi. Aliheshimiwa sana na Wayahudi wenzake wengi, kwa sababu alifanya kazi kwa manufaa ya watu wake na kutetea ustawi wa Wayahudi wote.

Iliyochaguliwa sasa

Esta 10: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia