Kutoka 25:1-9
Kutoka 25:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli wanipe michango ya matoleo, nawe upokee kwa niaba yangu. Utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu. Utapokea matoleo yafuatayo: Dhahabu, fedha, shaba, sufu ya buluu, ya zambarau na nyekundu, kitani safi iliyosokotwa manyoya ya mbuzi; ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, ngozi za mbuzi, mbao za mjohoro, mafuta kwa ajili ya taa, viungo kwa ajili ya mafuta ya kuweka wakfu na kwa ajili ya ubani wenye harufu nzuri, vito vya sardoniki, na vito vingine kwa ajili ya mapambo ya kizibao cha kuhani na kifuko cha kifuani. Vilevile Waisraeli watanitengenezea hema takatifu, ili niweze kukaa kati yao. Utatengeneza hema hiyo na vifaa vyake kulingana na mfano nitakaokuonesha.
Kutoka 25:1-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, fedha na shaba, na nyuzi rangi za buluu, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mjohoro, na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani. Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa samani zake zote, ndivyo mtakavyovifanya.
Kutoka 25:1-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu. Sadaka utakayopokea mikononi mwao ni hii; dhahabu, na fedha, na shaba, na nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na za rangi nyekundu, na nguo za kitani safi, na singa za mbuzi; na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, na miti ya mshita, na mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka, na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri; na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani. Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya.
Kutoka 25:1-9 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. “Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: “dhahabu, fedha na shaba; nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi; ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo; mbao za mshita; mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezo kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kizibau na kile kifuko cha kifuani. “Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. Tengeneza Maskani hii na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonesha.