Kutoka 36:3
Kutoka 36:3 Biblia Habari Njema (BHN)
Hao wakapokea kutoka kwa Mose vitu vyote vilivyotolewa na Waisraeli kwa hiari kwa ajili ya kazi ya hema takatifu. Watu waliendelea kumletea michango yao ya hiari kila asubuhi.
Kutoka 36:3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi.
Kutoka 36:3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
nao wakapokea mkononi mwa Musa matoleo yote, ambayo hao wana wa Israeli walikuwa wameyaleta kwa ajili ya huo utumishi wa mahali patakatifu, ili wapatengeneze. Kisha wakamletea matoleo kila siku asubuhi kwa moyo wa kupenda.
Kutoka 36:3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
nao wakapokea mkononi mwa Musa matoleo yote, ambayo hao wana wa Israeli walikuwa wameyaleta kwa ajili ya huo utumishi wa mahali patakatifu, ili wapafanye. Kisha wakamletea matoleo kila siku asubuhi kwa moyo wa kupenda.