Kutoka 40:34-35
Kutoka 40:34-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, lile wingu likalifunika lile hema la mkutano, na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukalijaza hema. Mose alishindwa kuingia ndani ya hema la mkutano kwa sababu hilo wingu lilikaa juu yake, na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ukajaa humo.
Kutoka 40:34-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani. Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.
Kutoka 40:34-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu. Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu.
Kutoka 40:34-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)