Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 7:1-13

Ezekieli 7:1-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Na wewe, mwanadamu, Bwana MUNGU aiambia hivi nchi ya Israeli; Ni mwisho; mwisho umezijia pembe nne za nchi. Sasa mwisho huu unakupata, nami nitakuletea hasira yangu, nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote. Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja. Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja. Ajali yako imekujia, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani. Basi hivi karibu nitamwaga ghadhabu yangu juu yako, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote. Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, napiga. Angalia, siku hiyo; angalia, inakuja; ajali yako imetokea; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka. Udhalimu umeinuka, ukawa fimbo ya uovu; hapana mtu atakayesalia miongoni mwao, wala katika jamii yao, wala kitu katika utajiri wao; wala hakutakuwa kutukuka kati yao. Majira yamewadia, siku ile inakaribia; huyo anunuaye asifurahi, wala asihuzunike auzaye; maana ghadhabu imewapata wote jamii. Kwa maana auzaye hatakirudia kilichouzwa, wajapokuwa wangali hai; kwa sababu maono haya yawahusu wote jamii; hapana mmoja atakayerudi; wala hapana mtu atakayejitia nguvu katika uovu wa maisha yake.

Shirikisha
Soma Ezekieli 7

Ezekieli 7:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: “Wewe mtu, waambie wakazi wa nchi ya Israeli kuwa mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Sasa ni mwisho! Mwisho umeifikia nchi yote kutoka pande zote nne! Sasa mwisho umewafikia; sasa mtausikia ukali wa hasira yangu juu yenu. Nitawahukumu kadiri ya mwenendo wenu. Nitawaadhibu kwa machukizo yenu yote. Sitawaachia wala sitawahurumia; nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu, maadamu machukizo bado yapo kati yenu. Ndipo mtakapotambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu. Ninachosema mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ni hiki: Mtapatwa na maafa mfululizo! Mwisho umekuja! Naam, mwisho umefika! Umewafikia nyinyi! Enyi wakazi wa nchi hii, maangamizi yenu yamewajia! Wakati umekuja; naam, siku imekaribia. Hiyo ni siku ya msukosuko na siyo ya sauti za shangwe mlimani. Sasa mtausikia uzito wa hasira yangu juu yenu. Nitawahukumu kulingana na mwenendo wenu; nitawaadhibu kadiri ya machukizo yenu. Sitawaachilia wala sitawaonea huruma. Nitawaadhibu kulingana na mienendo yenu maadamu machukizo yapo bado miongoni mwenu. Ndipo mtakapotambua kuwa ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayewaangamiza. “Tazameni, siku ile inakuja! Maangamizi yenu yamekuja. Ukatili uko kila mahali na kiburi kimechanua. Ukatili unaendelea kuwa mbaya zaidi. Hakuna hata mmoja wenu atakayebaki, wala vitu mlivyojirundikia kwa wingi au utajiri wenu; hatakuwako mtu mwenye heshima miongoni mwenu. Wakati umewadia, naam, ile siku imekaribia. Mnunuzi asifurahi wala mwuzaji asiomboleze; kwa sababu ghadhabu yangu itaukumba umati wote. Wauzaji hawataweza kurudia mali yao waliyouza hata kama wakibaki hai. Kwani maono haya yahusu umati wote na hayatabatilishwa. Kutokana na uovu huo, hakuna mtu atakayesalimisha maisha yake.

Shirikisha
Soma Ezekieli 7

Ezekieli 7:1-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Na wewe, mwanadamu, Bwana MUNGU aiambia hivi nchi ya Israeli; Ni mwisho; mwisho umezijia pembe nne za nchi. Sasa mwisho huu unakupata, nami nitakuletea hasira yangu, nitakuhukumu kulingana na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote. Jicho langu halitakuachilia, wala sitaona huruma; bali nitakupatiliza njia zako, na machukizo yako yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Bwana MUNGU asema hivi; Ni jambo baya, jambo baya la namna ya peke yake; angalia, linakuja. Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja. Ajali yako imekujia, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani. Basi hivi karibu nitamwaga ghadhabu yangu juu yako, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote. Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, BWANA, napiga. Angalia, siku hiyo; angalia, inakuja; ajali yako imetokea; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka. Udhalimu umeinuka, ukawa fimbo ya uovu; hapana mtu atakayesalia miongoni mwao, wala katika jamii yao, wala kitu katika utajiri wao; wala hakutakuwa kutukuka kati yao. Majira yamewadia, siku ile inakaribia; huyo anunuaye asifurahi, wala asihuzunike auzaye; maana ghadhabu imewapata watu wote. Kwa maana auzaye hatakirudia kilichouzwa, wajapokuwa wangali hai; kwa sababu maono haya yawahusu watu wote; hapana mmoja atakayerudi; wala hapana mtu atakayejitia nguvu katika uovu wa maisha yake.

Shirikisha
Soma Ezekieli 7

Ezekieli 7:1-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Neno la BWANA likanijia kusema: “Mwanadamu, hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo kwa nchi ya Israeli: Mwisho! Mwisho umekuja juu ya pembe nne za nchi. Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza. Sitawaonea huruma wala sitawarehemu, hakika nitalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA. “Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa yanakuja. Mwisho umewadia! Mwisho umewadia! Umejiinua wenyewe dhidi yenu. Umewadia! Maangamizi yamekuja juu yenu, ninyi mnaoishi katika nchi. Wakati umewadia, siku imekaribia, kuna hofu kuu ya ghafula, wala si furaha, juu ya milima. Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenu na kumaliza hasira yangu dhidi yenu, nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo. Sitawaonea huruma wala sitawarehemu; nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA ambaye huwapiga kwa mapigo. “Siku imefika! Imewadia! Maangamizi yamezuka ghafula, fimbo imechanua majivuno yamechipua! Jeuri imeinuka kuwa fimbo ya kuadhibu uovu, hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa, hata mmoja wa kundi lile, hakuna utajiri, hakuna chenye thamani. Wakati umewadia, siku imefika. Mnunuzi na asifurahi wala muuzaji asihuzunike, kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote. Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai, kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake.

Shirikisha
Soma Ezekieli 7