Mwanzo 14:22-23
Mwanzo 14:22-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, aliyeumba mbingu na dunia, kwamba sitachukua uzi au kamba ya kiatu, wala chochote kilicho chako, usije ukajivuna na kusema kwamba umenitajirisha.
Mwanzo 14:22-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi, ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala chochote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu
Mwanzo 14:22-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi, ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu
Mwanzo 14:22-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’