Mwanzo 39:11-12
Mwanzo 39:11-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku moja, Yosefu aliingia nyumbani kufanya kazi yake kama kawaida, na wafanyakazi wengine hawakuwamo nyumbani. Basi, mke wa Potifa alimshika joho lake na kumwambia, “Lala na mimi!” Lakini Yosefu akamwachia vazi lake mikononi mwake, akakimbilia nje.
Mwanzo 39:11-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Siku moja Yosefu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwepo na mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia.
Mwanzo 39:11-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani afanye kazi yake, na hapakuwa na mtu yeyote kati ya wale wa nyumbani karibu; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.
Mwanzo 39:11-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.