Waebrania 5:7-10
Waebrania 5:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu alipokuwa anaishi hapa duniani, kwa kilio kikuu na machozi, alisali na kumwomba Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kumwokoa kifoni; naye alisikilizwa kwa sababu ya kumcha Mungu. Lakini, ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, alijifunza kutii kwa njia ya mateso. Na alipofanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii, naye Mungu akamteua kuwa kuhani mkuu kwa utaratibu wa ukuhani wa Melkisedeki.
Waebrania 5:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii; kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 5:7-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Katika siku za maisha ya Yesu hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu. Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata, na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii. Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 5:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)