Yakobo 1:26-27
Yakobo 1:26-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe. Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.
Yakobo 1:26-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Yakobo 1:26-27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu. Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
Yakobo 1:26-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.