Yakobo 2:10-13
Yakobo 2:10-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunja sheria yote. Maana yuleyule aliyesema: “Usizini,” alisema pia “Usiue.” Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, wewe umeivunja sheria. Basi, semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. Maana, Mungu hatakuwa na huruma atakapomhukumu mtu asiyekuwa na huruma. Lakini huruma hushinda hukumu.
Yakobo 2:10-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
Yakobo 2:10-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru. Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
Yakobo 2:10-13 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote. Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria. Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru. Kwa kuwa hukumu bila huruma itatolewa kwa mtu yeyote asiyekuwa na huruma. Huruma huishinda hukumu.