Yakobo 2:2-4
Yakobo 2:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Tuseme mtu mmoja ambaye amevaa pete ya dhahabu na mavazi nadhifu anaingia katika mkutano wenu, na papo hapo akaingia mtu maskini aliyevaa mavazi machafu. Ikiwa mtamstahi zaidi yule aliyevaa mavazi ya kuvutia na kumwambia: “Keti hapa mahali pazuri,” na kumwambia yule maskini: “Wewe, simama huko,” au “Keti hapa sakafuni miguuni pangu,” je, huo si ubaguzi kati yenu? Je, na huo uamuzi wenu haujatokana na fikira mbaya?
Yakobo 2:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Wewe keti hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Wewe simama pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo maovu?
Yakobo 2:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavazi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavazi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu?
Yakobo 2:2-4 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Je, ikiwa mtu anakuja katika kusanyiko lenu akiwa amevaa pete ya dhahabu na mavazi mazuri, na kisha akaingia mtu maskini aliyevaa mavazi yaliyochakaa. Mkimpa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,” je, hamjabagua kati yenu wenyewe na kuwa mahakimu wenye mawazo maovu?