Yeremia 44:16-17
Yeremia 44:16-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno lile ulilotuambia kwa jina la BWANA, sisi hatutakusikiliza. Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.
Yeremia 44:16-17 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina la BWANA! Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama vile sisi na baba zetu, wafalme wetu na maafisa wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote.
Yeremia 44:16-17 Biblia Habari Njema (BHN)
“Jambo hilo ulilotuambia kwa niaba ya Mwenyezi-Mungu hatutalitii. Lakini kila kitu tulichoapa kufanya tutafanya: Tutamfukizia ubani malkia wa mbinguni na kummiminia tambiko ya kinywaji kama tulivyokuwa tunafanya sisi wenyewe na wazee wetu, wafalme wetu na viongozi wetu, katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Ama wakati huo tulikuwa na chakula tele, tulistawi na hatukuona janga lolote.
Yeremia 44:16-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)