Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 44:16-17

Yeremia 44:16-17 SRUV

Neno lile ulilotuambia kwa jina la BWANA, sisi hatutakusikiliza. Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.

Soma Yeremia 44