Yobu 26:1-4
Yobu 26:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha Yobu akajibu: “Aa! Jinsi gani ulivyomsaidia asiye na uwezo! Jinsi gani ulivyomwokoa asiye na nguvu! Jinsi gani ulivyomshauri asiye na hekima, na kumshirikisha ujuzi wako! Lakini umetamka hayo kwa ajili ya nani? Nani aliyekusukuma kuongea hivyo?”
Yobu 26:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu! Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi! Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
Yobu 26:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu! Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima! Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi! Je! Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
Yobu 26:1-4 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kisha Ayubu akajibu: “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu! Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima? Nayo ni busara gani kubwa uliyoonesha! Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?