Methali 24:23-29
Methali 24:23-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri. Anayemwachilia mtu mwenye hatia, hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa. Lakini wanaowaadhibu waovu watapata furaha, na baraka njema zitawajia. Jibu lililo la haki, ni kama busu la rafiki. Kwanza fanya kazi zako nje, tayarisha kila kitu shambani, kisha jenga nyumba yako. Usishuhudie bure dhidi ya jirani yako, wala usiseme uongo juu yake. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda! Ni lazima nilipize kisasi!”
Methali 24:23-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Makabila ya watu watamlaani, taifa watamchukia. Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia. Aibusu midomo atoaye jawabu la haki. Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako. Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako. Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.
Methali 24:23-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Amwambiaye mtu mwovu, Wewe una haki; Kabila za watu watamlaani, taifa watamchukia. Bali kwao wakemeao furaha itakuwako; Na baraka ya kufanikiwa itawajilia. Aibusu midomo atoaye jawabu la haki. Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako. Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako. Usiseme, Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; Nitamlipa mtu huyo sawasawa na tendo lake.
Methali 24:23-29 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonesha upendeleo katika hukumu si vyema: Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” makabila ya watu watamlaani, na mataifa watamkana. Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao. Jawabu la uaminifu ni kama busu la mdomoni. Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako. Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”