Methali 24:30-34
Methali 24:30-34 Biblia Habari Njema (BHN)
Nilipitia karibu na shamba la mvivu; shamba la mzabibu la mtu mpumbavu. Nilishangaa kuona limemea miiba, magugu yamefunika eneo lake lote, na ukuta wake wa mawe umebomoka. Nilitazama, nikawaza, mwishowe nikapata funzo: Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo! Kunja mikono yako tu upumzike! Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini, umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara kama mtu mwenye silaha.
Methali 24:30-34 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nilipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Niliona, nikapata mafundisho. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Methali 24:30-34 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. Kumbe! Lote pia limemea miiba; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Methali 24:30-34 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili, miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka. Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona: Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.