Methali 24:7-12
Methali 24:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa; penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo. Afikiriaye kutenda maovu daima ataitwa mtu mwenye fitina. Mpango anaofikiria mpumbavu ni dhambi; mwenye dharau huchukiwa na kila mtu. Ukifa moyo wakati wa shida, basi wewe ni dhaifu kweli. Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure; usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia. Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako!
Methali 24:7-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni. Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu; Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu. Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache. Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Methali 24:7-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni. Mtu afikiriye kutenda maovu, Watu watamwita mtundu; Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu. Ukizimia siku ya taabu, Nguvu zako ni chache. Uwaokoe wanaochukuliwa ili wauawe; Nao walio tayari kuchinjwa uwaopoe. Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?
Methali 24:7-12 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Hekima i juu mno kwa mpumbavu, katika kusanyiko langoni hana lolote la kusema. Yeye apangaye mabaya atajulikana kama mtu wa hila. Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka. Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo! Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni. Mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?