Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 6:1-19

Methali 6:1-19 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako, ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi kwa ajili ya mwingine, kama umetegwa na ulichosema, umenaswa kwa maneno ya kinywa chako, basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru, kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako: Nenda ukajinyenyekeshe kwake; msihi jirani yako! Usiruhusu usingizi machoni pako, usiruhusu kope zako zisinzie. Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji, kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji. Ewe mvivu, mwendee mchwa; zitafakari njia zake ukapate hekima! Kwa maana yeye hana msimamizi, wala mwangalizi, au mtawala, lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaamka lini kutoka usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika: hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha. Mtu mbaya sana na mlaghai, ambaye huzungukazunguka na maneno ya upotovu, ambaye anakonyeza kwa jicho lake, anayetoa ishara kwa miguu yake na kuashiria kwa vidole vyake, ambaye hupanga ubaya kwa udanganyifu moyoni mwake: daima huchochea fitina. Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula; ataangamizwa mara, pasipo msaada. Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA, naam, viko saba vilivyo chukizo kwake: macho ya kiburi, ulimi udanganyao, mikono imwagayo damu isiyo na hatia, moyo uwazao mipango miovu, miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu, shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo, na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.

Shirikisha
Soma Methali 6

Methali 6:1-19 Biblia Habari Njema (BHN)

Mwanangu, kama umejitolea kumdhamini jirani yako, ikiwa umetoa ahadi yako kwa ajili ya mtu huyo, umejibana kwa maneno yako mwenyewe, umejinasa kwa ahadi uliyofanya. Ujue kwamba uko chini ya mamlaka ya mwenzio, lakini mwanangu, ukitaka kujiokoa, basi fanya hivi: Mwendee mtu huyo mara moja umsihi akupe uhuru wako. Jitahidi usiache macho yako yapate usingizi, wala kope za macho yako zisinzie. Jiokoe kwa kujitoa katika mtego huo, mithili ya paa ama ndege amtorokavyo mwindaji. Ewe mvivu! Hebu ukamchungulie sisimizi, fikiria namna yake ya kuishi ukapate hekima. Sisimizi hana kiongozi, ofisa, wala mtawala; lakini hujiwekea chakula wakati wa kiangazi, hujikusanyia akiba wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hapo mpaka lini? Utaamka lini katika usingizi wako? Wasema: “Acha nilale kidogo tu, acha nisinzie kidogo! Niache nikunje mikono nipumzike kidogo!” Wakati huo umaskini utakuvamia kama mnyanganyi, ufukara utakufuata kama jambazi. Mtu mwovu, mtu asiyefaa kitu, huzururazurura akisema maneno mapotovu. Hukonyeza jicho kuwakosesha wengine, huparuza kwa nyayo, na kuashiria watu kwa vidole. Akiwa amejaa ulaghai moyoni hutunga maovu, huzusha ugomvi kila mahali. Kutokana na hayo maafa yatamvamia ghafla, ghafla atadhurika vibaya asiweze kupona tena. Kuna vitu sita anavyochukia Mwenyezi-Mungu; naam, vitu saba ambavyo ni chukizo kwake: Macho ya kiburi, ulimi mdanganyifu, mikono inayoua wasio na hatia, moyo unaopanga mipango miovu, miguu iliyo mbioni kutenda maovu, shahidi wa uongo abubujikaye uongo, na mtu achocheaye fitina kati ya ndugu.

Shirikisha
Soma Methali 6

Methali 6:1-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepeana mikono, Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako, Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe, Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako. Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego. Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana kiongozi, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hadi lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha. Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotovu. Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake. Mna upotovu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi. Basi msiba utampata kwa ghafla; Ghafla atavunjika, bila njia ya kupona. Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Shirikisha
Soma Methali 6

Methali 6:1-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa rafiki yako, Ikiwa wewe na mgeni mmepana mikono, Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako, Sasa, mwanangu, fanya hivi ukajiokoe, Kwa kuwa umejitia mkononi mwa jirani yako; Nenda ukanyenyekee, na kumsihi jirani yako. Usiache macho yako kupata usingizi, Wala kope za macho yako kusinzia. Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego. Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha. Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake. Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima, Hupanda mbegu za magomvi. Basi msiba utampata kwa ghafula; Ghafula atavunjika, bila njia ya kupona. Kuna vitu sita anavyovichukia BWANA; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.

Shirikisha
Soma Methali 6