Zaburi 18:1-3
Zaburi 18:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nakupenda wewe, Ee BWANA, nguvu yangu. BWANA ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu. Ninamwita BWANA anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
Zaburi 18:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Nakupenda, ee Mwenyezi-Mungu, nguvu yangu! Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu na mkombozi wangu; Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu za wokovu wangu na ngome yangu. Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa maadui zangu.
Zaburi 18:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe, BWANA, nguvu yangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. Namwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.
Zaburi 18:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe, BWANA, nguvu zangu, nakupenda sana; BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa, Hivyo nitaokoka na adui zangu.