Zaburi 36:5-7
Zaburi 36:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni. Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawaokoa wanadamu na wanyama. Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Zaburi 36:5-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Upendo wako, Ee BWANA, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee BWANA, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.
Zaburi 36:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Fadhili zako ee Mwenyezi-Mungu zaenea hata mbinguni; uaminifu wako wafika mawinguni. Uadilifu wako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama Jinsi gani zilivyo bora fadhili zako! Wanadamu hukimbilia kivulini mwa mabawa yako.
Zaburi 36:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hadi mawinguni. Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama. Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.