Zaburi 37:16-26
Zaburi 37:16-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Afadhali mali kidogo ya mtu mwadilifu kuliko utajiri wa watu waovu wengi. Maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Mwenyezi-Mungu huwategemeza waadilifu. Mwenyezi-Mungu hutunza maisha ya watu waaminifu, na urithi wao utadumu milele. Hawataaibika zikifika nyakati mbaya; siku za njaa watakuwa na chakula tele. Lakini waovu wataangamia, maadui za Mwenyezi-Mungu watanyauka kama maua nyikani; naam, watatoweka kama moshi. Mtu mwovu hukopa bila kurudisha; lakini mwadilifu hutoa kwa ukarimu. Waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi, lakini waliolaaniwa naye watafutiliwa mbali. Mwenyezi-Mungu huziongoza nyayo za mtu, humlinda yule ampendezaye. Ajapoanguka, haanguki akabaki chini, kwa sababu Mwenyezi-Mungu humtegemeza. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula. Daima huwapa wengine kwa furaha na kukopesha, na watoto wake ni baraka.
Zaburi 37:16-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi. Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki. BWANA huwatunza waaminifu, Na urithi wao utakuwa wa milele. Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka. Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. Maana waliobarikiwa na BWANA watairithi nchi, Nao waliolaaniwa naye watakatiliwa mbali. Hatua za mtu mwema huimarishwa na BWANA, Naye huipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, Maana BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.
Zaburi 37:16-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kidogo alicho nacho mwenye haki ni bora Kuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi. Maana mikono ya wasio haki itavunjika, Bali BWANA huwategemeza wenye haki. BWANA anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele. Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao BWANA watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka. Asiye haki hukopa wala halipi, Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu. Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi, Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa. Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA, Naye aipenda njia yake. Ajapojikwaa hataanguka chini, BWANA humshika mkono na kumtegemeza. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha, Na mzao wake hubarikiwa.
Zaburi 37:16-26 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Bora kidogo walicho nacho wenye haki kuliko wingi wa mali ya waovu wengi; kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, lakini Mwenyezi Mungu humtegemeza mwenye haki. Mwenyezi Mungu anazifahamu siku za wanyofu, na urithi wao utadumu milele. Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. Lakini waovu wataangamia: Adui za Mwenyezi Mungu watakuwa kama uzuri wa mashamba, watatoweka, watatoweka kama moshi. Waovu hukopa na hawalipi, bali wenye haki hutoa kwa ukarimu. Wale wanaobarikiwa na Mwenyezi Mungu watairithi nchi, bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali. Kama Mwenyezi Mungu akipendezwa na njia ya mtu, yeye huimarisha hatua zake, ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Mwenyezi Mungu humtegemeza kwa mkono wake. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula. Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. Watoto wao watabarikiwa.