Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 42:1-11

Zaburi 42:1-11 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)

Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu. Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu usiku na mchana, huku watu wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” Mambo haya nayakumbuka ninapoimimina nafsi yangu: Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, kwa kelele za shangwe na za shukrani katikati ya umati wa watu waliosherehekea. Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa kuwa bado nitamsifu, Mwokozi wangu na Mungu wangu. Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; kwa hiyo nitakukumbuka kutoka nchi ya Yordani, katika vilele vya Hermoni, kutoka Mlima Mizari. Kilindi huita kilindi, katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; mawimbi yako yote pamoja na viwimbi vimepita juu yangu. Mwenyezi Mungu huelekeza upendo wake mchana, wimbo wake uko nami usiku: maombi kwa Mungu wa uzima wangu. Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, “Kwa nini umenisahau? Kwa nini niendelee kuomboleza, nikiteswa na adui?” Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali adui zangu wanaponidhihaki, wakiniambia mchana kutwa, “Yuko wapi Mungu wako?” Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? Weka tumaini lako kwa Mungu, kwa kuwa bado nitamsifu, Mwokozi wangu na Mungu wangu.

Shirikisha
Soma Zaburi 42