Zaburi 78:56-72
Zaburi 78:56-72 Biblia Habari Njema (BHN)
Hata hivyo walimjaribu na kumwasi Mungu Mkuu; wala hawakuzingatia masharti yake. Ila waligeuka na kufanya mabaya kama wazee wao; wakayumbayumba kama upinde usio imara. Walimkasirisha kwa madhabahu zao za miungu; wakamchochea aone wivu kwa sanamu zao za kuchonga. Mungu alipoona hayo, akawaka hasira; akamkataa Israeli katakata. Aliyaacha makao yake kule Shilo, makao ambamo alikaa kati ya watu. Aliiacha ishara ya nguvu yake itekwe, utukufu wake utiwe mikononi mwa maadui. Aliwakasirikia watu wake mwenyewe; akawatoa waangamizwe kwa upanga. Moto ukawateketeza vijana wao wa kiume, na wasichana wao wakakosa wachumba. Makuhani wao walikufa kwa upanga, wala wajane wao hawakuomboleza. Kisha Bwana aliamka kama kutoka usingizini, kama shujaa aliyechangamshwa na divai. Akawatimua maadui zake; akawatia aibu ya kudumu milele. Lakini aliikataa jamaa ya Yosefu, wala hakulichagua kabila la Efraimu. Ila alilichagua kabila la Yuda, mlima Siyoni anaoupenda. Alijenga hapo hekalu lake kubwa kama mbingu, kama dunia aliyoiweka imara milele. Alimchagua Daudi, mtumishi wake, akamtoa katika kazi ya kuchunga kondoo. Alimtoa katika kazi ya kuchunga kondoo na wanakondoo, awe na jukumu la kuchunga watu wa Yakobo taifa lake. Achunge Israeli, watu wake Mungu mwenyewe. Daudi akawafunza kwa moyo wake wote, akawaongoza kwa uhodari mkubwa.
Zaburi 78:56-72 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini walimjaribu Mungu Aliye Juu, wakamwasi, Wala hawakuzishika shuhuda zake. Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakayumba kama upinde usiofaa. Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu, Wakamtia wivu kwa sanamu zao. Mungu alisikia, akaghadhibika, Akamkataa Israeli kabisa. Akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu; Akaziacha nguvu zake kutekwa, Na fahari yake mkononi mwa mtesi. Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga; Akaughadhibikia urithi wake. Moto ukawala vijana wao, Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, Makuhani wao walianguka kwa upanga, Wala wajane wao hawakuomboleza. Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele kwa sababu ya mvinyo; Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma, Akawatia aibu ya milele. Ila akaikataa hema ya Yusufu; Wala hakuichagua kabila la Efraimu. Bali aliichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni alioupenda. Akajenga patakatifu pake kama vilele, Kama dunia aliyoiweka imara milele. Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake. Akawahudumia kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.
Zaburi 78:56-72 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini walimjaribu Mungu Aliye juu, wakamwasi, Wala hawakuzishika shuhuda zake. Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakaepea kama upinde usiofaa. Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu, Wakamtia wivu kwa sanamu zao. Mungu akasikia, akaghadhibika, Akamkataa Israeli kabisa. Akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu; Akaziacha nguvu zake kutekwa, Na fahari yake mkononi mwa mtesi. Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga; Akaughadhibikia urithi wake. Moto ukawala vijana wao, Wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, Makuhani wao walianguka kwa upanga, Wala wajane wao hawakuomboleza. Ndipo Bwana alipoamka kama aliyelala usingizi, Kama shujaa apigaye kelele sababu ya mvinyo; Akawapiga watesi wake akawarudisha nyuma, Akawatia aibu ya milele. Ila akaikataa hema ya Yusufu; Wala hakuichagua kabila ya Efraimu. Bali aliichagua kabila ya Yuda, Mlima Sayuni alioupenda. Akajenga patakatifu pake kama vilele, Kama dunia aliyoiweka imara milele. Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake. Akawalisha kwa ukamilifu wa moyo wake, Na kuwaongoza kwa busara ya mikono yake.
Zaburi 78:56-72 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini wao walimjaribu Mungu, na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, wala hawakuzishika sheria zake. Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, wakawa wasioweza kutegemewa kama upinde wenye kasoro. Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao. Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa. Akaiacha hema ya Shilo, hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu. Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui. Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake. Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, makuhani wao waliuawa kwa upanga, wala wajane wao hawakuweza kulia. Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo. Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele. Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu, lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda. Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele. Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake. Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.