Ufunuo 12:1-2
Ufunuo 12:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, ishara kubwa ikaonekana mbinguni: Mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake! Alikuwa mjamzito, naye akapaza sauti kwa maumivu na uchungu wa kujifungua mtoto.
Ufunuo 12:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji la nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia, akiwa na uchungu na kuumwa katika kuzaa.
Ufunuo 12:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
Ufunuo 12:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kukaonekana ishara kuu mbinguni: Palikuwa na mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ukiwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa kichwani mwake. Alikuwa na mimba naye akilia kwa uchungu kwa kuwa alikuwa anakaribia kuzaa.