Ufunuo 9:20-21
Ufunuo 9:20-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wanadamu waliobakia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kutembea. Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wizi wao.
Ufunuo 9:20-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika mapigo hayo, bado walikataa kutubia kazi za mikono yao na hawakuacha kuabudu mashetani na sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea. Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao.
Ufunuo 9:20-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanadamu wengine waliobaki ambao hawakuuawa na mabaa hayo, hawakutubu na kuviacha vitu walivyokuwa wametengeneza kwa mikono yao wenyewe; wala kuacha kuabudu pepo, sanamu za dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia wala kutembea. Wala hawakutubu na kuacha kufanya mauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.
Ufunuo 9:20-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wanadamu waliosalia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kuenenda. Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wivi wao.