Soma Biblia Kila Siku 1Mfano
Mateso ya mgonjwa tuliyesoma habari zake tunaweza kuyaelewa japo kidogo tukizingatia muda aliougua – miaka 38! Mfumo wa tiba na taratibu za kijamii na kidini havikumsaidia. Kibaya zaidi, hata hakuna aliyemtambua kwamba na yeye alikuwapo. Katika kulalama kwake anasema hana mtu wa kumtia birikani. Yesu akamwona, kwa huruma akampoya ugonjwa wake. Baadaye akamwonya pia asitende dhambi tena. Fikiri maisha yako. Ni wapi umeugua na kushindwa? Mtegee Yesu sikio lako, ndiye jibu lako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 1 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz