Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Zaburi hii yaonyesha picha ya Bwana kama mchungaji mwema kwa namna isiyosahaulika. Mwimba Zaburi asemapo, Bwana ndiye mchungaji wangu(m.1), anashuhudia kuwa ana uhusiano wa binafsi naye. Hakika Bwana yu mchungaji mwema. Hujishugulisha sana na mahitaji ya kondoo wake. Akisha kumpa chakula kizuri na kinywaji kizuri humhakikishia usalama, wema, fadhili na makao ya milele (m.2, 4 na 6). Zaburi hii hutukumbusha kuwa Yesu ni mchungaji mwema, kama alivyosema mwenyewe: “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo” (Yn 10:7-11). Je, Yesu ni mchungaji wako pia?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz