Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Zaburi hii imetungwa na Daudi, na inahusu uhusiano kati ya mwenye haki na asiye haki. Inaonyesha hasa ule uchungu anaopata mwenye haki anapoona asiye haki akifanikiwa katika mambo yake. Daudi anasisitiza kwamba mwenye haki asijaribu kujipatia haki na kushinda kwa kutumia silaha na tabia ya asiye haki. Bali silaha yake na tabia yake iwe kumkabidhi Bwana njia yake na kuwa na upole! Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya, usiwahusudu ... ukae kimya mbele za Bwana, nawe umngoje kwa saburi ... wenye upole watairithi nchi (m.1, 7 na 11).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz