Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Somabiblia Kila Siku 3Mfano

Somabiblia Kila Siku 3

SIKU 6 YA 31

Yesu hakuja kuleta wokovu kwa Wayahudi tu bali kwa wanadamu wote. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye(Yn 3:16-17)! Sasa aliona dalilikwamba muda umefika atakapokufa kwa ajili ya wote. Maana waliotaka kumwona ni Wayunani, yaani, wacha Mungu ambao si Wayahudi (m.20-24). Tendo la Mariamu vilevile lilikuwa dalili kwa Yesu kwamba kifo chake kinakaribia (m.7-8). Yesu ni ile chembe ya nganoitakayokufa ardhini ili kutoa mazao mengi. Yaani kifo chake msalabani kitaleta wokovu kwa watu wote (m.32)! Pia kwako msomaji!

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Somabiblia Kila Siku 3

SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana