Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 16 YA 30

Huu ni mwujiza mkubwa wa Bwana. Aliifanya bahari kuwa nchi kavu, yaani maji yaligawanyika! Waisraeli walipita baharini kwenye nchi kavu. Jeshi la Farao liliwafuatia. Ila Mungu hakuwasaidia Wamisri kufika ng’ambo kama alivyowasaidia Waisraeli. Bali walikufa wote baharini. 1 Wakorintho 10:1-6 inaeleza juu ya kupita baharini kwa Waisraeli: Ndugu  zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; wote wakala chakula kile kile cha roho; wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani. Walitoka utumwani Misri na kuelekea nchi waliyoahidiwa na Mungu. Na sisi katika ubatizo tumetoka utumwani mwa Shetani na kuingia ufalmeni mwa Yesu. Ila bila imani hatuwezi kumpendeza.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana