Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 4Mfano

Soma Biblia Kila Siku 4

SIKU 6 YA 30

Leo twasoma yaliyoamriwa na Mungu kuhusu Pasaka. Pasaka ya Wana wa Israeli ni kielelezo cha Pasaka ya Wakristo. Jambo la msingi ni damu ya mwana-kondoo. Hiyo damu waliagizwa kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu. Maana ya ile damu iliyotiwa inasomeka katika m.13: Ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga nchi ya Misri. Hivyo Waisraeli waliokoa maisha yao. Sisi pia tunayo damu ya namna hii. Damu ya Kristo iliyomwagika Golgotha. Kuitia kwao milangoni ile damu ya mwana-kondoo kulikuwa ni kielelezo kwetu cha kumwamini Yesu na damu yake iliyolipa deni la dhambi zetu!

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 4

Soma Biblia Kila Siku 4 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka, na 1 Wathesalonike, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.

More

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana