Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hatua Sita Ya Uongozi Bora ZaidiMfano

Six Steps To Your Best Leadership

SIKU 6 YA 7

Hatari Unayohitaji Kuchukua

Ikiwa wewe ni kijana, u katika chuo kikuu, unafanya kazi, ama umestaafu, wakati huu ni wakati mwafaka kuchukua hatari. Chukua hatari unapokua na unapopungua. Hakuna aliyewahi kutekeleza chochote kwa kuwa mwangalifu. 

Sikuambii uchukue hatari katika mambo mabaya. Usihatarishe uhusiano mzuri, usihatarishe afya yako, na usiharibu vitu vinavyoendelea vizuri. Lakini, una nadharia ipi? Unapuuza dhana ipi? Unashikilia vichocheo vipi kwa dhati? Chukua hatari katika imani. 

Ninapenda yale ambayo Rais Mstaafu Jimmy Carter alisema, “Nenda katika tawi, pale ni ambapo pana matunda.” 

Pengine umesikia kuhusu mfanyabiashara tajiri lakini pengine mlaghai katika Biblia ambaye alipanda tawi ili kuweza kumwona Yesu. Alijulikana kuwa mroho kama mtozaushuru mkuu, na alipata utajiri wake kupitia sifa hiyo. Siku moja alihatarisha heshima yake na maisha yake kwa kupanda mti halisi ili kumwona Yesu. Yesu alimwona Zakayo, akajialika katika nyumba yake, na maisha ya Zakayo ilibadilika papo hapo kuwa tajiri zaidi. 

Ikiwa unataka kuwa mtu ambaye kamwe umekuwa, fanya ambayo umekuwa ukifanya. Ikiwa unataka kubadili wewe ni nani, badili unachofanya. Yaani, kubadilisha matunda maishani mwako, pengine utahitaji kuenda katika tawi.

Unahitaji kuanza kuandika kitabu, kumwwomba mtu umchumbie, kuanzilisha bidhaa, kuanzisha huduma, kuanza kuenda kanisa, kuanza tangazo, ama kitu kinginecho? Kutegemea kile ambacho Mungu anakuelekeza kufanya, ni hatari ipi unahitaji kuchukua?

Tenda: Mwambia mtu unayemwamini kuhusu hatari ambayo unataka kuchukua. Kisha, chukua hatua ya kwanza.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Six Steps To Your Best Leadership

U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.

More

Tungependa kushukuru Craig Groeschel na Life.Church kwa ajili ya kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.craiggroeschel.com/