Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Paulo alizidi kuwapenda wasafiri wenzake. Bila shaka alikuwa amewaombea sana kwa Mungu. Na Mungu aliwapa neno la tumaini kwa kupitia mtumishi wake Paulo (m.21-26). Sasa wakamsikiliza sana Paulo (taz. m.35-36:Alipokwisha kusema hayo akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula. Ndipo wakachangamka wote, wakala chakula wenyewe) na ikatokea kama alivyokuwa ametabiri. Wote wakasalimika (m.44b:Watu wote wakapata kuifikilia nchi kavu salama). Kuna maneno yanayoeleweka zaidi kwa tafsiri ya Biblia Habari Njema: “tukadiriki” (m.16) = tuliwahi kuokoa kabla hayajaharibika.“fungu liitwalo Sirti” (m.17) = ufuko wa bahari, pwani ya Libya. “hori yenye ufuo” (m.39) = ghuba moja yenye ufuko.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz