Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TISAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TISA

SIKU 1 YA 7

  

MARIAMU NA MARTHA

Ikawa Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakienda Yerusalemu, akaingia kwenye kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani kwake.

Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Maria, ambaye yeye aliketi chini miguuni mwa Yesu akisikiliza yale aliyokuwa akisema.

Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike.

Martha akaja kwa Yesu na kumwuliza,

“Bwana, hujali kwamba ndugu yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.”

Lakini Bwana akamjibu, 

"“Martha, Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi?Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.”

"

siku 2

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA TISA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI-Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org