Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 8Mfano

Soma Biblia Kila Siku 8

SIKU 14 YA 31

Waisraeli wote wamejumlishwa kwenye agano lake Mungu, wamo chini ya baraka au laana zake. Mtu asijidanganye kwa kuiendea miungu mingine akidai kuwa hakuna shida kwa kuwa yumo ndani ya agano la amani. Hakika ataonja laana zake Bwana (m. 18-21: Asiwe mtu katikati yenu ... ageukaye moyo wake leo amwache Bwana, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga; ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu; Bwana hatamsamehe mtu huyo, lakini wakati huo hasira ya Bwana na wivu wake vitafuka moshi juu ya mtu yule, na laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki itamkalia juu yake, na Bwana atalifuta jina lake chini ya mbingu. Bwana atamtenga kwa uovu, kutoka kabila zote za Israeli, kwa laana zote za agano lililoandikwa katika chuo hiki cha torati). Na vizazi vijavyo vitakapouliza kwa nini taifa la Israeli lilipelekwa kifungoni, jibu ni, Ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, … wakaenda wakatumikia miungu mingine (m.24-26). Hata leo linamchukiza sana Mungu mtu akimwacha na kutegemea miungu batili. 

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz