Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/20

SIKU 18 YA 29

Ulimwengu ulilaaniwa dhambi ilipoingia Mauti, magonjwa na maovu ya kila aina yamesababishwa na laana hiyo. Yesu Kristo ameiondoa laana akichukua dhambi za watu wote na kufanywa laana badala yao. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona(Isa 53:4-5). Katika Yesu kuna uponyaji, kiroho na kimwili. Uponyaji wa mwili hatuuoni sana hapa duniani. Wapo wanaoponywa kwa mwujiza hapa hapa, ila wengine wataiona Mbinguni. Na wote hufa. Lakini tunaamini ufufuo wa mwili! Baadaye ushindi tulio nao katika Kristo utakamilika kwetu kabisa! Sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake (Flp 3:20-21).

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana